Fresh Kenyan News|Tuesday, June 18, 2013
You are here: Home » Entertainment » Theatre » Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • Follow Us!

Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo! 



Wapo binadamu sampuli tofauti. Vita sinavyo kwa yeyote maana’ke pawapo na vita, basi ukweli hutiwa dhalamani na hivyo kuyeyushwa pasi na lengo. Huruma ninayo, na hilo sitolijutia kamwe; Huruma tena komavu – Huruma yenye mashiko na ya kudumu … Kwenu nyie Wakenya!

Kwa maoni yangu, aghalabu mja ni kiumbe razini mwenye hadhi na uwezo wa kubaini mambo halali na yale batili, lakini sivyo walivyo wakenya. Miye ‘si’ Mkenya ela nilizaliwa na n’naishi Kenya. Wapo wapingao msimamo huu wangu eti sababu kuwa nilizaliwa, nikapewa malazi mumu humu Kenya na hatima’ye kitambulisho nikakipata,

Wakenya Mlivyo1 253x190 Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!

Nyie Wakenya

eti nafaa kujivunia kuwa Mkenya: Mwanzo hilo la kitambulisho lilinipenyeza kwingi tena kwa siku ayami. Leo kwa kasisi, kesho kwa mlezi, mtondo kwa jirani … mtondogoo; na hatimaye? Eti maisha ni ‘nipe nikupe’.

Ni Katika Kenya tu Ambamo, Ufanisi maishani hugomelewa kwenye stashahada na shahada alizo nazo mtu. Kwenu wakenya, wingi na ukubwa wa vijikaratasi hutaswiriwa sawia na upana wa ubongo na labda, nd’o sababu kuu ya kuwepo kwa watu wazimu afisini zetu. Kila mmoja huwa mbumbumbu kwenye ajira, na yendapo mvange, hapo ndio utimamu humvaa. Najuwa nitakashifiwa au labda kunikashifu umeshaanza nisemapo akina Dada wa Kenya wamejawa na ulegevu, upotovu na upepetevu wa maadili kiasi cha hata kutembea nusura tuputupu! – Kama kwamba wanaume wa Kenya ni gumegume tu, mabinti zetu kunyakuliwa kwa wepesi na watanashati was’o na lolote la ‘Ukenya’ wala Kenya.

Wajuzi na Mabingwa

Wakenya nyie ni wajuzi na mabingwa kwa hakika. Hebu nambie, Nchi gani nyingine ambamo neno ‘Otherwise’ hutumiwa kumsabahi mtu? Wapi huko kila swala hugeuzwa mzaha isipokuwa Kenya? Shambulizi liwapo Nchini, kila mmoja hulifanyia mzaha lisiwe la kuliza wala la kutamausha.

Werevu wenu huwatia najisi na hivyo kuwafisha fedheha machoni pa wengi. Juzi juzi tu, Mkenya Alex Kinyua aliyeishi Nchini Amerika, alifumaniwa akijishtakia njaa kwa bongo na nyoyo za watu, na hilo halikupita bila uboresho wa stihizai, wapo walosema hivi; “Ujinga ni kuuliza Alex Kinyua kama anapenda bongo flava…”

Mbinu nzuri ya kubaini mkenya halisi, ni kwa kuyapa sikio maneno ya sentensi zao, eti, “Me I love NewYork… “Me I donno why people hate him…”. Neno la kwanza kulitamka, huwa ni la utani pekee… Jingine la kutamausha, ni mnavyoupa ulevi hadhi. Hudhani ndo wakwanza kuwa ulevini; hilo nina hakika nalo. Hulonga “Man, it was dope! Kuwasha nayo.”… ‘nayo’ limekuwa kibwagizo katika kila maongezi. Kila jambo limekuwa la kinyume; kula, ketembea, uongozi na hata msemapo. Badala ya kusema ‘Mtu wangu’ werevu wenu huwazuga kusema, “mtu wangu-Mtu nguyaz, niaje-nijeaz, iko wapi-iko piwa.”

Ni wakenya tu ndo hutohoa kila silabi ili kupata maana ‘wanayoifahamu’ fika. Waulize wengi sababu ya kutumia; smh, sic!, lol. Lmfao na vidude vya sura kwenye kila ujumbe na watakutumbulia macho kama kwamba we’ u mzawa wa Ahera.

Ipo dhana kuwa kila anayesafiri nje ya mipaka ya Kenya, hwenda ‘Majuu.’ Mtu asafiripo Uganda, “ako majuu.” Endapo Somalia, “ako majuu.” Ni Humu Kenya tu [Aghalabu Barabara kuu ya Thika] ambapo askari wa trafiki huwa na mkao wa sekunde zisizo zidi tano, kisha wanabadilishina vitanga na kusanzuka.

Ni humu nchini tu, ambapo usalama wa mwananchi huwa na insi mwenyewe tu. Popote mtu alipo, hujitakirimu na usalama wake awezavyo. Ahadi za askari na serikali walimo, huwa ni za siku kadha tu wala si kadhaa. Hata kwenye maabadi, usalama umekuwa njozi ambayo ukomo wayo hautabiriki. Wezi mnao kwa hakika; na uwoga pia. Vipi bastola moja iwafyatishe waumini zaidi ya ishirini? Dah! Simba waoga!

Akili Kichwani!

 Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!

Related posts:

Share and Enjoy

  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!
  • wp socializer sprite mask 32px Werevu wajinga; Wakenya Mlivyo!

Leave a Response

Email
Print